- 382 viewsDuration: 3:25Wizara ya Elimu hatimaye imewakusanya na kuwapeleka shule wanafunzi wa Gredi ya 10 katika mtaa wa Mukuru kwa Njenga jijini Nairobi ambao walikuwa wameshindwa kuripoti shuleni kwa kukosa karo na pesa za mahitaji mengine. Zoezi hilo linafuatia taarifa ya runinga ya Citizen katika eneo hilo iliyobaini kuwa wanafunzi 25 walikuwa bado hawajajiunga na shule kutokana na changamoto za kifedha.