Wizara ya fedha yatoa malipo kulipa madeni ya nyumba za bei nafuu

  • | K24 Video
    159 views

    Katika njia tatanishi wizara ya fedha imetoa malipo ya shilingi bilioni tisa nukta nane kulipa madeni ya nyumba za bei nafuu na za idara ya polisi pamoja na shilingi milioni mia mbili kumi na saba katika idara ya marekebishob licha ya kamati inayochunguza madeni ya shilingi bilioni mia sita kubaini iwapo ni halali au haramu. Hatua hiyo inayokinzana na msimamo wa rais William Ruto kuwa ni sharti madeni yote yachunguzwe imejiri wakati ambapo mdhibiti wa bajeti margaret nyakango anadai wizara ya fedha inaitisha fedha bila kutoa stakabadhi zote hitajitika. Ripoti ya ofisi hiyo vilevile imebainisha jinsi shilingi milioni sabini na tano zililipwa kukabiliana na nzige ambazo wanakamati wa fedha wanaamini hawakuonekana nchini katika kipindi hicho.