- 961 viewsDuration: 4:22Unapozungumzia wizi wa mifugo, wengi hudhani ni visa vinavyotokea tu kwa jamii za wafugaji ila ni uhalifu unaowasibu wengi. Katika kaunti ya Migori, wizi wa mifugo umekuwa tisho kubwa kwa wakazi ambao mbali na kupoteza mifugo, wengine pia wameuawa kwenye uhalifu huo. Walter Nyambaga alikuwa Migori ambako alibaini kuwa wakaazi wengine sasa wameamua kulala kwenye zizi la ng'ombe kuchunga mifugo wao.