Zaidi ya watu 100 wafariki katika ajali ya boti Nigeria

  • | BBC Swahili
    260 views
    Takriban watu 106 wamefariki dunia nchini Nigeria baada ya mashua kupinduka kwenye mto Niger siku ya Jumatatu. Abiria hao 300 walikuwa wakisafiri kutoka Kwara kuelekea jimbo la Niger kwa ajili ya kuhudhuria harusi. Watu 144 wameokolewa lakini wengine bado hawajulikani walipo. Ajali za mashua ni za kawaida nchini Nigeria, kwa kawaida husababishwa na mizigo kupita kiasi, matengenezo duni, au mafuriko wakati wa msimu wa mvua. #bbcswahili #nigeria #mafuriko