Janga la maafa limekumba ziwa Baringo katika kaunti ya Baringo kwa mara nyingine huku familia kadhaa, shule, mashamba na hoteli zilizo karibu na ziwa zikifurika maji kutokana na kupanda kwa kiwango cha maji ya ziwa hilo. Haya yanafuatia mvua kubwa iliyonyesha eneo hilo ambapo ziwa Baringo lilivunja kingo zake na maji kufurika kwenye maeneo ya karibu ukiwemo uharibifu wa miundomsingi kwenye eneo la ziwa hilo. Hali hiyo imesababisha wakazi kushambuliwa na wanyama kama vile mamba na viboko ambao wamevutwa na mkondo wa maji na kukaribia makazi ya wenyeji.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive