
121 views
Gavana wa Marsabit ataka hatua za dharura kukabiliana na janga la kibinadamu
Gavana wa Kaunti ya Marsabit ameelezea masikitiko yake kuhusu janga la kibinadamu katika eneo hilo kufuatia kuingia nchini kwa wakimbizi 50,000 wanaotoroka vita nchini Ethiopia. Gavana huyo amesema familia nyingi zimeachwa katika hali ngumu huku watu 22 wakijeruhiwa na wengine wawili kufariki kutokana na risasi zilizopotea katika eneo hilo la mpaka. Gavana Mahmud amesema milipuko ya vilipuzi pia imeripotiwa katika maeneo ya makazi ya raia, ikiwemo karibu na vituo vya huduma za umma, na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi, hasa watoto. Aidha, shughuli za mitihani ya kitaifa zimetatizika pamoja na utoaji wa huduma muhimu. Ameliomba serikali kuimarisha usalama, huku akitaka vilipuzi ambavyo havijalipuka viondolewe na wataalamu waliohitimu.
- Latifa Akumu murder suspects remanded for 21 more days
- IEBC warns of KSh 12 billion budget shortfall ahead of 2027 polls
- EACC to name candidates with questionable integrity ahead of 2027 polls
- Ruto awashutumu viongozi wa upinzani kwa kuchochea vijana kufanya fujo
- Tafakari Ya Babu: Mjinga na Mpumbavu
- Watu watano wauawa katika uvamizi wa wezi wa mifugo Isiolo
- “2024 Finance Bill was eventually passed, and there was no harm to our nation,” President Ruto says
- Amriya Super Cup yazinduliwa Mombasa kuwaepusha vijana na mihadarati wakati wa likizo