
129 views
Mahakama ya Siaya yasitisha kufurushwa kwa wajumbe saba wa NEC ya FKF
Mahakama Kuu mjini Siaya imetoa maagizo ya kusimamishwa kwa utekelezaji wa azimio lililopitishwa na mkutano maalum wa Shirikisho la Soka Kenya, FKF, uliowatimua wajumbe saba wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya shirikisho hilo. Katika kesi iliyowasilishwa na mjumbe wa NEC kutoka Pwani, Gabriel Mghendi, mahakama ya Siaya pia imetoa amri inayozuia FKF, maafisa wake, mawakala, vyombo au watu wanaofanya kazi chini ya mamlaka yake kutangaza wazi, kujaza au kuchukua nafasi za wanachama hao saba wa NEC. Kesi hiyo itatajwa tarehe 20 Novemba 2026 kwa maagizo zaidi. Shirikisho la Soka Kenya liliwabandua wanachama saba wa Kamati Kuu ya NEC tarehe 7 Novemba, katika mkutano maalum uliokumbwa na machafuko katika Kaunti ya Meru.
- Latifa Akumu murder suspects remanded for 21 more days
- IEBC warns of KSh 12 billion budget shortfall ahead of 2027 polls
- EACC to name candidates with questionable integrity ahead of 2027 polls
- Ruto awashutumu viongozi wa upinzani kwa kuchochea vijana kufanya fujo
- Tafakari Ya Babu: Mjinga na Mpumbavu
- Watu watano wauawa katika uvamizi wa wezi wa mifugo Isiolo
- “2024 Finance Bill was eventually passed, and there was no harm to our nation,” President Ruto says
- Amriya Super Cup yazinduliwa Mombasa kuwaepusha vijana na mihadarati wakati wa likizo