
62 views
Kenya Police FC yaichapa Posta Rangers 2-1 licha ya kubaki na wachezaji kumi
Kenya Police FC walipata pointi tatu muhimu baada ya kuichapa Posta Rangers 2-1, katika mechi ya Ligi Kuu ya FKF katika uwanja wa Police Sacco, huku polisi wakimaliza na wachezaji kumi kwa sehemu kubwa ya kipindi cha pili. Nana Asante alifungua mlango wa mabao kwa polisi dakika ya 33 kabla ya Erick Zakayo kuongeza la pili dakika ya 36. Hata hivyo, polisi walipunguzwa idadi ya wachezaji na kubaki na wachezaji kumi dakika ya 39 baada ya Kevin Ongele kuonesha kadi nyekundu ya moja kwa moja. Posta Rangers walifanikiwa kupunguza pengo la magoli dakika ya 71 kupitia Mark Shaban, lakini hawakuweza kupata goli la kusawazisha matokeo.
- Latifa Akumu murder suspects remanded for 21 more days
- IEBC warns of KSh 12 billion budget shortfall ahead of 2027 polls
- EACC to name candidates with questionable integrity ahead of 2027 polls
- Ruto awashutumu viongozi wa upinzani kwa kuchochea vijana kufanya fujo
- Tafakari Ya Babu: Mjinga na Mpumbavu
- Watu watano wauawa katika uvamizi wa wezi wa mifugo Isiolo
- “2024 Finance Bill was eventually passed, and there was no harm to our nation,” President Ruto says
- Amriya Super Cup yazinduliwa Mombasa kuwaepusha vijana na mihadarati wakati wa likizo