
324 views
Kanisa la Kianglikana laonya dhidi ya misimamo mikali kuhusu mageuzi ya uchaguzi
Kanisa la Kianglikana sasa linaitaka Tume ya Uchaguzi nchini IEBC kuangazia masuala tata yanayoibuliwa ili kuzuia mtafaruku. Askofu wa kanisa hilo Dayosisi ya Garissa, Francis Omondi, ametoa wito kwa wanasiasa na tume ya uchaguzi kutoa nafasi kwa mazungumzo ili kuangazia masuala tata ya mabadiliko yanayopendekezwa. Askofu Omondi ameonya dhidi ya misimamo mikali ambayo huenda ikayumbisha taifa, chini ya miezi tisa kabla ya uchaguzi mkuu. Amezungumza baada ya ibada maalum ya kuweka wakfu kwa mapadri na mashemasi wa kanisa hilo Kaunti ya Garissa.
- Latifa Akumu murder suspects remanded for 21 more days
- IEBC warns of KSh 12 billion budget shortfall ahead of 2027 polls
- EACC to name candidates with questionable integrity ahead of 2027 polls
- Ruto awashutumu viongozi wa upinzani kwa kuchochea vijana kufanya fujo
- Tafakari Ya Babu: Mjinga na Mpumbavu
- Watu watano wauawa katika uvamizi wa wezi wa mifugo Isiolo
- “2024 Finance Bill was eventually passed, and there was no harm to our nation,” President Ruto says
- Amriya Super Cup yazinduliwa Mombasa kuwaepusha vijana na mihadarati wakati wa likizo