Aliyekuwa mgombea mwenza wa Odinga atishia kesi Afrika Mashariki

  • | Citizen TV
    18,297 views

    Aliyekuwa mgombea mwenza wa Kinara wa Azimio Raila Odinga, Martha Karua sasa anasema wanafikiria kuwasilisha kesi katika mahakama ya haki ya Afrika Mashariki kupinga uamuzi wa mahakama ya upeo nchini, ulioafiki ushindi wa William Ruto kuwa rais wa tano wa jamuhuri ya Kenya. Karua aliyezungumza eneo la Kimunye kaunti ya Kirinyaga pia ameahidi kuhakikisha kuwa serikali inayoingia ya Rais Mteule Wiliam Ruto inatekeleza majukumu yake inapasavyo. Naye kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka akizungumza kaunti ya Machakos akisema ni wakati wa wakenya kumpa fursa Ruto kuongoza taifa na kutimiza ahadi zake kwa wakenya