- 66,043 viewsDuration: 2:12Muungano wa kimataifa wa wanasheria na makundi ya haki za binadamu umeiomba rasmi Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kumchunguza rais wa Tanzania, na serikali yake kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu unaodaiwa kufanywa wakati wa uchaguzi Mkuu wa hivi karibuni. Waraka wa Ombi kwa ICC linamtuhumu Rais Samia Suhulu Hassan na maafisa wengine wa ngazi za juu kwa kuhusishwa moja kwa moja na vifo vya raia wakati wa maandamano ya baada ya uchaguzi. Juma lililopita Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alizindua tume ya uchunguzi kuhusu vurugu hizo baada ya kuwatuhumu wapinzani na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kusababisha machafuko. - - #bbcswahili #tanzania #maandamano #uchaguzi2025