Skip to main content
Skip to main content

Washukiwa wapewa zawadi kituoni Central Mombasa

  • | Citizen TV
    4,264 views
    Duration: 1:50
    Huku sherehe za krismasi zikiendelea ulimwenguni kote, wakristo, serikali na mashirika ya kijamii yametakiwa kuwakumbuka watu wa mapato ya chini pamoja na wanaorandaranda mitaani kama njia mojawapo ya kuonyesha upendo. Akizungumza na wanahabari jijini Mombasa kwenye hafla ya kuwapa chakula washukiwa katika kituo cha polisi cha Central pamoja na familia za watu wanaorandaranda mitaani, afisa msimamizi wa kituo hicho Koplo Mwanza Kulola, amesema kuwa kando na msimu wa sherehe ipo haja kwa jamii kuwasaidia watu hao ikizingatiwa kuwa tayari wengi wao wamekosa matumaini maishani.