- 2,171 viewsDuration: 1:43Vigogo wa chama cha ODM wameendelea na semi za kumuunga mkono Rais William Ruto kwa muhula wa pili, wakitoa onyo kali dhidi ya wale waliosema ni mahasidi wanaojaribu kutia shubiri kwenye chungwa. Akizungumza katika eneo bunge la Suna East, kinara wa chama hicho Oburu Oginga, amesema kuwa sharti chama cha chungwa kiwe katika serikali mwaka 2027 na kuwa watafanya kila wawezalo kufanikisha azma hiyo. Kwa upande wake, rais William Ruto amesema kuwa ataungana na viongozi walio na rekodi ya utendakazi huku akiwarushia vijembe wanasiasa wa upinzani. rais Ruto aliambatana na mawaziri pamoja na viongozi kutoka eneo la Nyanza ambapo walihudhuria hafla ya michezo iliyoandaliwa na mbunge wa Suna east Junet Mohamed katika shule ya Kadika kaunti ya Migori