Skip to main content
Skip to main content

Maelfu wa wakazi wa Kilifi waukaribisha mwaka mpya katika tamasha la muziki na utamaduni

  • | Citizen TV
    984 views
    Duration: 2:30
    Ilikuwa ni tafrija ya kuvutia kwa maelfu ya wakaazi wa Kaunti ya Kilifi waliokusanyika kukaribisha Mwaka Mpya kwa kutumbuizwa na wasanii mbalimbali kutoka kaunti hiyo katika fainali ya kusaka vipaji kwenye tamasha la muziki lililolenga kukuza talanta za wenyeji pamoja na wasanii wajao kutoka kaunti nzima. Wasanii hao walisisimua umati kwa maonyesho ya kuvutia, pamoja na wanamuziki mashuhuri wa pwani, akiwemo msanii mashuhuri Susumila, na kuugeuza usiku huo kuwa sherehe ya kweli ya utamaduni, ubunifu, na uwezeshaji wa vijana. Viongozi tofauti kutoka Kaunti Hiyo walihudhuria wakiongozwa na Gavana Gideon Mung’aro, mbunge wa Malindi Amina Mnyazi sambamba na Katibu mkuu katika idara ya vijana na maswala ya uchumi bunifu Fikirini Jacobs.