11,664 views
Duration: 48s
Marais wa mataifa ya Afrika Mashariki wamewatoa ahadi za pesa kwa wachezaji wao wa kandanda wanaoshiriki katika michuano ya kandanda ya barani Afrika-CHAN.
Hii leo Rais Ruto wa Kenya ameahidi shilingi milioni 2.5 kwa kila mchezaji iwapo watashinda mechi yao dhidi ya Zambia. Kenya imeshawapa wachezaji wake shilingi milioni 2.5, sawia na dola 19,350 baada ya kuibuka washindi na kutoka sare katika mechi mbili za awali.
Tanzania nayo imetoa ahadi ya shilingi bilioni 1 ya Tanzania iwapo watashinda kinyanganyiro hicho, hiyo ni sawia na dola laki 4. Huku Rais Yoweri Museveni wa Uganda akitoa ahadi sawia na hiyo kwa timu yake.
Je, mtindo huu wa zawadi ya mamilioni ya Dedham utashawishi vipi matokeo ya CHAN?
@RoncliffeOdit anachambua kwa kina suala hili kwa pamoja na taarifa nyingine nyingi saa tatu usiku wa leo, mubashara kwenye Dira ya Dunia TV kupitia ukurasa wa YouTube, BBc Swahili.
-
-
#bbcswahili #tanzania #kenya #kandanda #soka #CHAN