- 7,555 viewsDuration: 1:58Vijana watatu kutoka Diani kaunti ya Kwale wamejisalimisha kwa maafisa wa polisi baada ya kuasi uhalifu wa makundi ya vijana wa Panga Boys. Watatu hao wamejiunga na wengine arobaini walioasi makundi hayo mwaka jana wakisema wamechukua mwelekeo huo ili kuhakikisha kuwa usalama wa mji wa Diani unaendelea kuimarika. Akiwapokea vijana hao kamanda wa polisi eno la Msambweni Robinson Lang'at amewataka vijana zaidi kujisalimisha huku akionya wazazi dhidi ya kupuuza majukumu yao ya kuwalea vijana kwa maadili.