- 340 viewsDuration: 1:23Waziri wa maji na unyunyiziaji mashamba Eric Mugaa amemwachisha kazi mwanakandarasi aliyekuwa akijenga Mtambo wa majitaka wa mji wa Meru eneo la Rwanyange kwa sababu ya utepetevu. Waziri Mugaa amesema mwanakandarasi huyo ambaye alianza ujenzi huo mwaka wa 2019 kwa gharama takriban shilingi Bilioni Moja, amejenga asilimia 25 tu za mradi huo licha ya kuahidi kumaliza kazi hiyo Desemba mwaka jana. Kulingana na Mugaa, serikali itatafuta mkandarasi mwingine wa kumalizia mradi huo.