Skip to main content
Skip to main content

Hali ya Hofu Tanzania: Africa Eye inachunguza wimbi la watu kutoweka

  • | BBC Swahili
    27,099 views
    Duration: 51:04
    #BBCAfricaEye inachunguza wimbi la watu kutoweka linaloeneza hofu kote Tanzania. Samia Suluhu alipokuwa rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania mwaka 2021, baada ya kifo cha ghafla cha mtangulizi wake akiwa madarakani, kulikuwa na matumaini kwamba urais wake ungesaidia kuvunja kwa utawala wa kiimla. Aliondoa marufuku ya mikutano ya vyama vya upinzani, akaruhusu vyombo vya habari kufanya kazi kwa uhuru zaidi, na akatoa wito wa ushirikiano na ujumuishaji mpana wa kisiasa. Hata hivyo, matumaini ya mabadiliko ya kudumu yalififia haraka. Kuanzia viongozi wa upinzani na watetezi wa haki za binadamu, hadi wasanii na hata wanachama wa chama tawala chenyewe, msako mkali usio na kifani dhidi ya wakosoaji wa serikali umeitikisa Tanzania. Kupitia ushuhuda mzito wa manusura wa utekaji nyara na mateso, Wakisimulia tena kwa undani mambo ya kutisha waliyopitia filamu hii inafichua kampeni ya vitisho na hofu ambayo wakosoaji wa serikali wanavumilia nchini. 00:00 Hali ya Hofu: Kutoweka kwa Kulazimishwa Tanzania 01:57 Ukweli mchungu nyuma ya taswira ya kidemokrasia 03:52 “Waumize wachache ili wengi waogope” 06:21 “Siku niliyotekwa” - Sativa 09:10 Utekaji si jambo jipya Tanzania 10:10 Samia Suluhu Hassan: urais wa matumaini? 13:03 “Kuangaza tochi machoni, unahisi kama macho yanatoka nje” 15:34 Wanaharakati mashuhuri wanaenda Tanzania kumuunga mkono kiongozi wa upinzani aliyefungwa 17:03 “Ni makosa gani niliyoyafanya?” 21:35 “Nilipoteza matumaini kabisa” 22:49 Walifanyiwa na watu waliovaa sare za polisi 24:19 Kuachwa kwenye pango la mbwa mwitu ili aliwe 29:35 Utekaji ambao haujapatiwa ufumbuzi unaochochewa na siasa 31:53 “Maumivu yalikuwa makali sana, sikuwa na machozi, mwili wangu uliingia kwenye mshtuko.” 38:16 “Lengo lao lilikuwa kuniua. Nisingepaswa kuwa hapa nikisimulia hadithi hii.” 40:05 “Kutoweka kwa kulazimishwa ni vigumu sana kuthibitisha Tanzania.” 44:57 “Huwezi kupata haki kupitia ukimya.” Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw