- 592 viewsDuration: 1:40Shirika la huduma za wanyamapori nchini, KWS, limedhibiti moto uliokuwa umezuka na kusambaa kwa kasi katika mbuga ya kitaifa ya ziwa Nakuru. Moto huo uliochukua zaidi ya saa sita kuzimwa ulizuka siku chache tu baada ya moto mwingine mkubwa kuzuka katika mbuga ya mlima Longonot. KWS ikiwaonya wakenya kujiepusha na kuwasha moto kiholela haswa wakati huu wa msimu wa kiangazi.