- 15,232 viewsDuration: 2:04‘Meli iliyokamatwa na dawa za Cocaine nchini El Salvador ilisajiliwa Zanzibar’ Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ameyasema hayo Februari 26, 2026, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Ikumbukwe kuwa, Februari 19, 2026, katika eneo la La Unión nchini El Salvador, Jeshi la Majini la taifa hilo lilitangaza kukamata meli iliyokuwa imebeba tani 6.6 za dawa za kulevya aina ya cocaine. Mzigo huo ulikuwa ukisafirishwa baharini, umbali wa takriban maili 380 kusini-magharibi mwa pwani ya bahari ya Pasifiki ya nchi hiyo. Kukamatwa kwa meli hiyo kunatajwa kuwa sehemu ya operesheni za kuimarisha mapambano dhidi ya usafirishaji haramu wa dawa za kulevya katika ukanda huo. - - #bbcswahili #dawazakulevya #tanzania #elsalvador #foryouシ Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw