- 23,184 viewsDuration: 53sWaziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameuambia mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba bado hajamaliza kupambana na Hamas. Wakati wa hotuba yake, baadhi ya wajumbe waliondoka ukumbini huku pia kukiwa na maadamano ya kutaka vikwazo dhidi ya Israel na mengine ya familia za mateka wanaotaka jamaa zao waachiliwe. Netanyahu pia amesema kutambuliwa kwa Palestina kama taifa huru ni kama wazimu mtupu. Amefanya hotuba yake wakati ambapo rais wa Marekani Donald Trump hatakubali Israel kukalia ukingo wa Magharibi. @RoncliffeOdit atakuwa na mengi zaidi katika Dira ya Dunia TV leo usiku. Pia tufuatilie kwenye ukurasa wetu wa YouTube BBC News Swahili - - #bbcswahili #israel #trump