Skip to main content
Skip to main content

Abiria wakwama zaidi ya saa sita kwenye barabara ya Nakuru–Nairobi

  • | Citizen TV
    8,292 views
    Duration: 1:16
    Mamia ya wasafiri walikwama kwa zaidi ya saa sita kwenye barabara kuu ya Nakuru - Nairobi usiku wa kuamkia leo kufuatia msongamano mkubwa wa magari. Msongamano huo wa magari ulishuhudiwa kwa muda katika maeneo ya kikopey, barnabas, kinungi na kimende. Baadhi ya abiria na maafisa wa usalama wakilaumu msongamano huo kutokana na madereva kutofuata sheria za barabarani. Wengi waliokuwa wakisafiri waliuwa wakirejea jijini Nairobi baada ya sherehe za krismasi.