Skip to main content
Skip to main content

Afisa wa GSU azuiliwa kwa tuhuma za mauaji Eldoret

  • | Citizen TV
    2,937 views
    Duration: 1:31
    Polisi mjini Eldoret wanamzuilia afisa wa GSU aliyehusishwa na mauaji ya mwanamke mmoja katika eneo la burudani la Kikosi cha GSU huko Naiberi, Uasin Gishu. Polisi hao wanasema mshukiwa huyo, Nathan Kirwa, ambaye ni mlinzi wa Gavana wa Uasin Gishu, anasubiri kufikishwa mahakamani kesho huku uchunguzi ukiendelea. Haya yakijiri huku familia ya mwanamke aliyeuawa ikitaka haki kwa mauaji yake. Familia ya marehemu Doris Murei inadai kuwa afisa huyo wa GSU alimvamia mwanamke huyo na kumuua baada ya kuzozana.