Skip to main content
Skip to main content

Afisa wa KWS atoa ushahidi kinzani katika kesi ya Brian Odhiambo

  • | Citizen TV
    831 views
    Duration: 1:17
    Mmoja wa maafisa sita wa Huduma kwa Wanyamapori nchini, KWS, ameiambia mahakama jinsi walivyomkamata kijana wakati wa kutoweka kwa mvuvi Brian Odhiambo mwaka jana. Hata hivyo, afisa huyo, Evans Kimaiyo, amekana kuwa kijana aliyekamatwa alikuwa Brian Odhiambo. Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu Mkuu wa Nakuru, Kipkurui Kibelion, Kimaiyo alionekana kutoa kauli kinzani na taarifa yake ya awali, ambapo alikiri kuwa alimuona Odhiambo akikamatwa na kuingizwa kwenye gari la polisi. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tarehe 20 mwezi huu.