- 293 viewsDuration: 3:24Kongamano la Afrika Forward limeidhinisha ushirikiano wa mataifa yaliyohudhuria kukabili changamoto zinazosababisha kuzorota kwa usalama kama vile ugaidi na mapinduzi ya serikali kukabiliwa kupitia nguvu za kiusalama. Aidha, marais wa Afrika waliokuwepo mkutanoni kupitia ushirikiano na Ufaransa wameapa kusikiza na kuangazia maswala yanayohusu vijana kama vile ukosefu wa ajira, kwa lengo la kuzuia ghasia na maandamano.