Ushirikiano kati ya kaunti umepewa kipaumbele kama suluhisho la kupunguza vifo vya wanawake wanaojifungua na watoto wachanga.
Data ya miezi saba tangu kuanzishwa kwa mpango huo inaonyesha kuwa asilimia 90 ya kaunti zote 47 sasa zinafanya mikutano ya kila wiki kutathmini mafanikio na changamoto. Kwa mujibu wa Baraza la Magavana kupitia idara ya afya, mpango huu unahusisha madaktari bingwa wa wanawake katika hospitali za kaunti, wakiratibu ufuatiliaji wa wajawazito kuanzia ujauzito hadi kujifungua.