Agizo la Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba kwamba taasisi za elimu ya juu ziendelee kutumia mfumo wa sasa wa ufadhili limezua sintofahamu vyuoni, huku wanafunzi wakitaka ufafanuzi kuhusu kiwango cha karo wanachopaswa kulipa.
Ogamba amesema mfumo huo utaendelea kutumika hadi Mswada wa Elimu ya Juu wa 2026 utakapopitishwa na Bunge na kuwezesha mabadiliko. Wakati huo huo, wasiwasi umeibuka kuhusu maelfu ya wanafunzi ambao tayari wameripoti katika taasisi za elimu ya juu bila fedha za kujikimu.
Serikali pia imetangaza kuongeza muda wa kutuma maombi ya ufadhili.