Skip to main content
Skip to main content

Uhuru Kenyatta aachia uongozi wa Jubilee baada ya uamuzi wa mahakama

  • | Citizen TV
    68,812 views
    Duration: 2:54
    Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta ametangaza kujiondoa afisini kama kinara wa Chama cha Jubilee, kufuatia uamuzi wa Jumatatu wa Mahakama Kuu ulioshikilia kuwa marais wastaafu hawaruhusiwi kushikilia nyadhifa zozote katika vyama vya kisiasa, miezi sita baada ya kuondoka afisini. Katika taarifa, Kenyatta hata hivyo amesema alisalia kileleni mwa Jubilee miaka minne baadaye kutokana na mgogoro wa uongozi chamani, ambao ulihitaji kusuluhishwa mahakamani kabla ya kuondoka kwake. Uamuzi huo uliotolewa na Jaji Lawrence Mugambi haujamzuia Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kushiriki katika siasa za humu nchini.