- 23,211 viewsDuration: 3:32Jioni ya leo tunaanza na taarifa kuhusu kutekwa nyara na kisha kuachiliwa kwa mhariri wa Standard Group, Alex Kiprotich, huku sasa ikibainika kuwa gari lililotumika katika tukio hilo linahusishwa na ofisi ya waziri mmoja wa serikali. Alex alitekwa nyara na kuzuiliwa kwa zaidi ya saa tano jana usiku katika eneo la Gilgil, kaunti ya Nakuru, kabla ya kuachiliwa karibu na bwawa la Masinga. Alex ameeleza namna alivyofunikwa uso kwa muda wote huo huku akiulizwa maswali kuhusu taarifa zake zinazohusu na kuikosoa serikali.