- 1,753 viewsDuration: 2:05Aliyekuwa seneta mteule wa Nairobi Millicent Omanga amewataka vijana na kina mama kumakinika katika uchaguzi wa viongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Akizungumza alipozuru hospitali ya uzazi ya Pumwani hapa jijini Nairobi, Omanga amesisitiza umuhimu wa wananchi kuchagua viongozi wanaoweza kushughulikia changamoto zinazowakabili. Aidha, ametupilia mbali ahadi za serikali za kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi, akikosoa pia uzinduzi wa ruwaza ya mwaka 2060 uliofanywa na rais william ruto, akisema kuna haja ya serikali kuweka mkazo kwanza katika kutimiza ahadi ilizotoa kwa wananchi.