Timu ya All Stars FC huko Luanda iliibuka mshindi wa mashindano ya nne ya mechi ya Harold Mbati Champions Cup iliyofanyika wikendi iliyopita. All Stars FC iliishinda Kima United mabao matatu kwa mawili kwenye mechi iliyochezwa katika uwanja wa Maseno Polytechnic Grounds, Luanda. Timu hii ikijishindia tuzo ya shilingi laki nne huku wengine wakipata tuzo za laki, mbili, laki moja na elfu hamsini. Kwenye tuzo za wachezaji Binafsi, mchezaji Wilson Kola wa Spurs FC walishinda tuzo ya mchezaji bora huku mwenzake Davies Obanda pia akituzwa. Washikadau mbalimbali kutoka nchini na kimataifa walihudhuria mechi hii ya nne ya Harold Mbati Champions Cup