Skip to main content
Skip to main content

Asasi za usalama zawaonya viongozi wachochezi

  • | Citizen TV
    964 views
    Duration: 3:05
    Asasi za serikali zinazohusika na usalama na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao zimeonya viongozi wenye ndimi za uchochezi dhidi ya kuwarejesha Wakenya kwenye machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Wakizungumza kwenye mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini, viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa IEBC, Erastus Ethekon, wameapa kukabiliana na wafadhili wa wahuni wanaovuruga amani kwenye mikutano ya kisiasa.