- 306 viewsDuration: 3:46John Mbinda, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Lodwar, amewataka vijana wanaotaka mabadiliko ya uongozi nchini kutumia njia za kidemokrasia badala ya kushiriki katika maandamano yenye vurugu. Amesema maandamano hayo yamesababisha vifo, majeraha na madai ya kutekwa nyara kwa baadhi ya raia, huku akisisitiza umuhimu wa amani, mazungumzo na kuheshimu utawala wa sheria katika kutatua tofauti za kisiasa.