- 28,218 viewsDuration: 3:17Hatua ya Gavana wa Siaya James Orengo kutangaza nia ya kuwania urais ndani ya mrengo wa Linda Mwananchi imeonekana kuleta tumbo joto miongoni mwa wanasiasa wa muungano huo, hasa wanaomuunga mkono Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. Hata hivyo, Orengo aliyezungumza na runinga ya Citizen amewakashifu wanaopinga azma yake, akisema ushindani ndani ya muungano huo ni ishara ya demokrasia. Baadhi ya viongozi wa muungano huo sasa wanasema uamuzi wa nani atakuwa mgombea tayari umefanywa.