- 448 viewsDuration: 4:49Takriban watoto elfu 14 huzaliwa na ugonjwa wa selimundu nchini kila mwaka huku changamoto za matibabu zikiendelea kushuhudiwa. Ugonjwa huo umeendelea kuwa miongoni mwa maradhi yanayoripotiwa kwa wingi huku baadhi ya familia za waathiriwa zikieleza wasiwasi kuhusu kile wanachosema ni ukosefu wa hatua za kutosha kutoka kwa serikali. Katika juhudi za kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa huo, baba mmoja ameanza safari ya kutoa elimu na uhamasisho kuhusu selimundu huku akimsaidia mwanawe anayeugua maradhi hayo baada ya kumpoteza mtoto mwingine kutokana na ugonjwa huo.