- 1,093 viewsDuration: 2:17Bajeti ya mwaka wa 2026/27 iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi imeibua hisia mseto miongoni mwa Wakenya. Wengi wakilalamika kuwa bajeti hiyo imeangazia zaidi utoaji wa huduma na maendeleo na kupuuza kumwondolea Mkenya wa kawaida mzigo mzito wa ushuru na gharama ya juu ya maisha. Aidha, baadhi wameisifia bajeti hiyo wakisema masuala muhimu kama vile elimu na mgao wa fedha kwa kaunti yameangaziwa ipasavyo. Kupunguzwa kwa fedha zitakazokopwa kufadhili bajeti pia kumeshabikiwa na baadhi ya Wakenya, huku wengine wakitaka kuzibwa kwa mianya ya utumizi mbaya wa pesa za umma.