Skip to main content
Skip to main content

Bandari ya Mombasa yakabiliwa na msongamano wa makontena kutokana na ongezeko la ushuru

  • | Citizen TV
    3,277 views
    Duration: 3:05
    Bandari ya Mombasa sasa inakabiliwa na hatari ya msongamano mkubwa wa makontena huku taarifa zikieleza kuwa wafanyabiashara wamesita kuondoa mizigo iliyowasili kutoka ng’ambo, hasa Uchina, kutokana na ongezeko la ushuru. Ushuru huo, ulioanza kutekelezwa Agosti 21, umeongeza gharama kutoka Sh2.5 milioni hadi Sh3.2 milioni. Mawakala wanaokusanya mizigo kwa niaba ya wafanyabiashara wanasema mgomo utaendelea hadi KRA ipunguze ushuru huo mpya.