- 28,221 viewsDuration: 2:14Kuingia kwenye mitaro iliyojaa vumbi, plastiki na takataka bila kulipwa hata sarafu moja, sio kazi inayopendwa na wengi. Lakini kwa Irene Mmbaga, binti mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa Dar es Salaam, hii ndiyo furaha na fahari yake. Akiongozwa na msukumo kutoka kwa mama yake, Irene amejitolea kutunza mazingira nchini Tanzania tangu utotoni, na kuchapisha maudhui yake katika mitandao ya kijamii. Amezungumza na Martha Saranga katika waridi wa BBC. #bbcswahili #waridiwabbc #wanawake Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw