- 3,699 viewsDuration: 3:24Mwanaharakati Bob Njagi hii leo alifikishwa katika Mahakama ya Kajiado baada ya kukamatwa Jumatano iliyopita, siku moja kabla ya maadhimisho ya kumbukumbu za maandamano ya Gen z. Baadaye mwanaharakati huyo aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja na Mahakama Kuu. Aidha faili ya kesi hiyo ilifungwa Kajiado na Njagi ametakiwa kufika katika mahakama kuu ya Nairobi baadaye mwezi huu kwa mwelekeo zaidi.