- 948 viewsDuration: 4:24Imebainika kuwa baadhi ya maafisa wa polisi na walimu katika Busia County wameathirika pakubwa na matatizo ya afya ya akili yanayotokana na msongo wa mawazo, huku visa vya kujitoa uhai vikitajwa kuongezeka. Suala hilo liliibuliwa wakati wa kongamano lililoandaliwa na maafisa wa afya kwa lengo la kutoa mafunzo kuhusu namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo na kuimarisha afya ya akili, hasa katika kipindi hiki cha changamoto za kiuchumi na kijamii.