CHAGUZI NDOGO OL KALOU
Kamati ya usalama ya kaunti ya Nyandarua imedai kwamba vyama vya kisiasa vinavyowania uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Ol Kalou, vinakiuka kanuni za Tume Huru ya Uchaguzi na Uratibu wa Mipaka (IEBC) kuhusu saa za kampeni. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Abdirisack Jaldesa, ambaye pia ni Kamishna wa Kaunti ya Nyandarua, aliwahimiza wagombea kuhakikisha wafuasi wao wanahitimisha mikutano yao kabla ya usiku kuwadia ili kudumisha usalama na utulivu wa umma. Akizungumza afisini mwake, Jaldesa alielezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la visa vya vurugu na uharibifu wa vifaa vya kampeni. Pia aliwashauri wagombea wote kuwajulisha polisi mapema kuhusu shughuli zao za kampeni ili kuweka mipango kabambe ya usalama.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive