- 4,803 viewsDuration: 1:47Chama cha DCP kimesema mbunge wa Mukurwe-ini John Kaguchia sasa hataomba msamaha kama alivyoagizwa na tume ya haki na uwiano kutokana na semi zake za chuki na uchochezi. Akizungumza kwenye ibada ya wafu katika kanisa la PCEA Giathugu huko Mukurwe-ini, kaunti ya Nyeri, Katibu mkuu wa chama hicho John Methu ameishutumu NCIC akidai inafanya ubaguzi kuhusiana na visa vya uchochezi. Kwa upande wake, Kaguchia amesema ataijibu NCIC baada ya kukamilika Kwa kesi iliyowasilishwa mahakamani dhidi yake.