- 1,460 viewsDuration: 59sChama cha Mawakili nchini Kenya, LSK kimeshtumu serikali kwa kile kinachotaja kama kutokosa mpango kuhusu bei ya mafuta na umeme. Chama hicho kinasema ongezeko la hivi karibu la bei ya mafuta na gharama zinazohusiana na umeme limewasukuma mamilioni ya Wakenya kuwa katika hali ngumu zaidi kiuchumi na kifedha. Rais wa LSK, Charles Kanjama, amesema Chama hicho pia kimesisitiza kuwepo kwa ukaguzi wa mfumo wa G2G, kikisema ni miongoni mwa sababu kuu zinazochangia kupanda kwa bei ya petroli nchini.