Skip to main content
Skip to main content

CHAUMA ni chama cha aina gani katika uchaguzi huu?

  • | BBC Swahili
    6,592 views
    Duration: 1:35
    Wakati Tanzania ikielekea katika uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mnamo Oktoba 29, Chama cha CHAUMA nacho kimezindua kampeni zake rasmi jana Jumapili katika uwanja wa Jangwani jijini Dar es Salaam. Huku ajenda kuu za chama hicho zikiwa ni Kupambana na rushwa kwa vitendo, Kuboresha huduma za afya na elimu kwa kila Mtanzania, Kurekebisha mfumo wa ajira kwa vijana, Kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha Watanzania wote. Lakini je CHAUMA ni chama cha aina gani katika uchaguzi huu? Je ndio kinaenda kuwa chama kikuu cha upinzani? @eze_kamwaga anatujuza ushawishi wa chama hiki nchini Tanzania. 🎥: @frankmavura - - #bbcswahili #chauma #siasa #tanzania #uchaguzi2025 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw