Skip to main content
Skip to main content

CHUO CHA UTALII CHA RONALD NGALA KUANZA MASOMO SEPTEMBA, WANAFUNZI 1,000 WATARAJIWA KUJIUNGA

  • | KNA Video
    12 views
    Duration: 2:58
    Chuo cha Utalii cha Ronald Ngala kinatarajiwa kuanza masomo rasmi mwezi Septemba, huku wanafunzi 1,000 wakitarajiwa kujiunga katika awamu ya kwanza. Ujenzi wa chuo hicho umefikia asilimia 95 na kinatarajiwa kuwa moja ya taasisi za kisasa zaidi za mafunzo ya utalii barani Afrika. Katibu wa Utalii Julius Bitok amesema chuo hicho kitasaidia kukuza sekta ya utalii na kuchangia lengo la Kenya la kupokea watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2028. Naye Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro amesema chuo hicho kitatoa fursa kwa wakazi wa Pwani kupata mafunzo na vyeti katika utalii, hoteli na uchumi samawati.