Skip to main content
Skip to main content

Claire Ochieng azungumzia maisha baada ya kushambuliwa kwa asidi

  • | Citizen TV
    81,682 views
    Duration: 5:45
    Kisa cha mwanamke aliyemwagiwa asidi barabarani kufuatia madai ya mzozo wa kimapenzi kilitikisa vichwa vya habari mapema mwaka huu. Mwathiriwa wa tukio hilo, Claire Ochieng, alichomeka vibaya na kulazwa hospitalini kwa muda kabla ya kwenda mafichoni. Afisa wa kitengo cha ujasusi Elvis Opiyo, ambaye yuko kizimbani, anadaiwa kuwakodi watu kumshambulia Claire kwa kumwagia asidi baada ya madai ya kutengana kwao. Miezi mitatu baada ya tukio hilo, Claire amevunja ukimya na kueleza maisha yake pamoja na changamoto anazopitia huku uchunguzi kuhusu tukio hilo ukiendelea.