- 8,632 viewsDuration: 3:41Mmiliki wa Karen Hospital Daktari Dan Gikonyo ambaye alimhudumia naibu rais Rigathi Gachagua kabla ya kutimuliwa kwake mamlakani, ametetea ushahidi wake kwa kuthibitisha kwamba mteja wake alilazwa katika hospitali yake. Aidha, Daktari Gikonyo alieleza majaji wanaosikiza kesi ya Gachagua ya kupinga kuondolewa kwake kama naibu rais kwamba alipokea simu kutoka kwa rais William Ruto akitaka kujua hali ya afya ya Gachagua wakati alifikishwa hospitalini kwa matibabu.