- 5,172 viewsDuration: 2:21Maafisa wa Directorate of Criminal Investigations wanaochunguza mauaji ya msichana Joy Kanini aliyepatikana ameuawa huko Nyeri wamekagua nyumba ya mshukiwa mkuu John Muriithi, anayeaminika kumuuwa msichana huyo, kuukata mwili wake vipande na kuvitupa katika maeneo tofauti kwenye barabara ya Ngangarithi. Katika nyumba hiyo, polisi walipata ushahidi muhimu unaoashiria kuwa mshukiwa alimuuwa msichana huyo ndani ya chumba hicho kabla ya kwenda kutupa mwili. Kama anavyoarifu Franklin Wallah, polisi wanawaomba wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kumkamata mshukiwa huyo ambaye ametoroka.