Viongozi wa chama cha DCP wamewataka wanasiasa wanaoiunga mkono serika kujibu Maswali yaliyoibuliwa na Kinara wa chama hicho Rigathi Gachagua, kwa kuwaeleza Wakenya kile ambacho serikali imefanikisha hadi sasa, ikilinganishwa na ahadi ilizotoa kabla ya kuingia madarakani. Viongozi hao pia wamekosoa matamshi ya Waziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi, kwamba ongezeko la ununuzi wa soda ni ishara kuwa Wakenya wana fedha zaidi mifukoni. Wamedai kuwa kauli hiyo haitoi taswira halisi ya kiuchumi na hali inayowakabili wananchi wa kawaida.