- 7,019 viewsDuration: 2:52Chama cha DCP kimeonya dhidi ya jaribio la kumkata Mbunge wa Manyatta, Gitonga Mukunji, kwa madai ya kuhusika katika kupanga vurugu zilizoshuhudiwa nje ya mkutano ulioongozwa na Naibu Rais Kithure Kindiki eneo la Nembure, Kaunti ya Embu. Wakizungumza katika Kanisa la ACK Witima huko Othaya, ambako walirejea miezi kadhaa baada ya kuvamiwa Januari mwaka huu, viongozi hao wametaja vurugu za Jumamosi kama mwiba wa serikali kujidunga, kufuatia kile walichokitaja kuwa utepetevu wake katika kukabiliana na wahuni. Kamau Mwangi anaarifu.